Genesis 46:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Yakobo akaondoka Beer-sheba. Wanawe wakamchukua yeye, watoto wao wachanga pamoja na wake zao katika magari ambayo Farao alipeleka kumchukua.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba, nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo, na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao alikuwa amempelekea kumsafirisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yakobo akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Yakobo akaondoka Beer-sheba. Wanawe wakamchukua yeye, watoto wao wachanga pamoja na wake zao katika magari ambayo Farao alipeleka kumchukua.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao aliyokuwa amempelekea kumsafirisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yakobo akaondoka Beer-Sheba nao wana wa Israeli wakamchukua baba yao Yakobo na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa yale Farao aliyokuwa amempelekea kumsafirisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yakobo akaondoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyotuma Farao ili kumchukua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Yakobo akaondoka Beer-sheba. Wanawe wakamchukua yeye, watoto wao wachanga pamoja na wake zao katika magari ambayo Farao alipeleka kumchukua.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yakobo alipoondoka Beri-Seba, wana wa Isiraeli wakampandisha baba yao Yakobo garini nao watoto wao na wake zao, ndiyo yale magari, Farao aliyoyatuma kumchukua.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yakobo akaondoka kutoka Beer-sheba; wana wa Israeli wakamchukua baba yao na watoto wao wadogo, na wake zao katika magari aliyoyapeleka Farao ili kumchukua.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yakobo akaondoka Beri-Seba. Wana wake wakamupeleka yeye, watoto wao wachanga pamoja na wake zao katika magari ambayo mufalme wa Misri alituma kwa kumubeba.