Genesis 47:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye chakula kiliadimika kabisa nchini kote. Njaa ilikuwa kali sana hata ikawafanya watu wote katika nchi ya Misri na ya Kanaani kudhoofika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, hapakuwa na chakula katika eneo lote; kwa kuwa njaa ilikuwa kali sana; Misri na Kanaani zote zikaharibiwa kwa sababu ya njaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala hapakuwa na chakula katika nchi yote, kwa kuwa njaa ilikuwa nzito sana, hata nchi ya Misri, na nchi ya Kanaani zikataabika, kwa sababu ya njaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye chakula kiliadimika kabisa nchini kote. Njaa ilikuwa kali sana hata ikawafanya watu wote katika nchi ya Misri na ya Kanaani kudhoofika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, hapakuwepo chakula katika sehemu yote kwa kuwa njaa ilikuwa kali sana; Misri na Kanaani zote zikaharibiwa kwa sababu ya njaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, hapakuwepo chakula katika sehemu yote kwa kuwa njaa ilikuwa kali sana; Misri na Kanaani zote zikaharibiwa kwa sababu ya njaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Baadaye hapakuwa na chakula katika nchi yote, kwa kuwa njaa ilikuwa kali sana, hata nchi ya Misri na nchi ya Kanaani zikataabika, kwa sababu ya njaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye chakula kiliadimika kabisa nchini kote. Njaa ilikuwa kali sana hata ikawafanya watu wote katika nchi ya Misri na ya Kanaani kudhoofika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Chakula hakikuwako katika nchi zote, kwa kuwa njaa ilikuwa nzito sana, nayo nchi ya Misri nayo nchi ya Kanaani zikaenda kuzimia kwa ajili ya njaa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala hapakuwa na chakula katika nchi yote, kwa kuwa njaa ilikuwa nzito sana, hata nchi ya Misri, na nchi ya Kanaani zikataabika, kwa sababu ya njaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma chakula kikakosekana kabisa katika inchi yote. Njaa ilikuwa kali sana hata ikawafanya watu wote katika inchi ya Misri na ya Kanana kukonda.