Genesis 47:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo wakamletea Yosefu mifugo yao: Farasi, ng'ombe, kondoo, mbuzi na punda, naye akawapa chakula. Mwaka huo Yosefu akawa anawapa chakula kwa kubadilishana na mifugo yao yote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo wakaleta mifugo yao kwa Yusufu, naye akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi, kondoo na mbuzi, ng’ombe, na punda wao. Katika mwaka huo wote Yusufu akawapa chakula kwa kubadilishana na mifugo yao yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaleta wanyama wao kwa Yusufu; Yusufu akawapa chakula badala ya farasi, na badala ya kondoo, na badala ya ng'ombe, na badala ya punda, naye akawalisha chakula badala ya wanyama wao wote mwaka ule.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo wakamletea Yosefu mifugo yao: farasi, ng'ombe, kondoo, mbuzi na punda, naye akawapa chakula. Mwaka huo Yosefu akawa anawapa chakula kwa kubadilishana na mifugo yao yote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo wakaleta mifugo yao kwa Yosefu, naye akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi zao, kondoo na mbuzi zao, ng'ombe na punda zao. Katika mwaka huo wote Yosefu akawapa chakula kwa kubadilishana na mifugo yao yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo wakaleta mifugo yao kwa Yusufu, naye akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi zao, kondoo na mbuzi zao, ng’ombe na punda zao. Katika mwaka huo wote Yusufu akawapa chakula kwa kubadilishana na mifugo yao yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaleta wanyama wao kwa Yusufu; Yusufu akawapa chakula kwa kubadilisha na farasi, kondoo, ng'ombe na punda, naye akawalisha chakula badala ya wanyama wao wote mwaka ule.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo wakamletea Yosefu mifugo yao: Farasi, ng'ombe, kondoo, mbuzi na punda, naye akawapa chakula. Mwaka huo Yosefu akawa anawapa chakula kwa kubadilishana na mifugo yao yote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, walipopeleka kwa Yosefu nyama, waliowafuga, naye Yosefu akawapa chakula kwa farasi wao na kwa makundi yao ya mbuzi na kondoo na kwa makundi yao ya ng'ombe na kwa punda wao; ndivyo, alivyowatunza mwaka huo na kuwapa chakula kwa makundi yao yote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaleta wanyama wao kwa Yusufu; Yusufu akawapa chakula badala ya farasi, na badala ya kondoo, na badala ya ng’ombe, na badala ya punda, naye akawalisha chakula badala ya wanyama wao wote mwaka ule.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu wakamuletea Yosefu nyama wao: farasi, ngombe, kondoo, mbuzi na punda, naye akawapa chakula. Mwaka ule Yosefu akakuwa anawapa chakula kwa kubadilishana na nyama wao wote.