Genesis 47:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ardhi ambayo Yosefu hakuinunua ni ile iliyomilikiwa na makuhani. Hao hawakulazimika kuiuza ardhi yao kwani waliishi kwa posho maalumu waliyopewa na Farao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo hakununua nchi ya makuhani, kwa sababu walipokea mgawo wao wa kawaida kutoka kwa Farao, nao walikuwa na chakula cha kuwatosha kutokana na mgawo waliopewa na Farao. Hii ndiyo sababu hawakuuza ardhi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ila nchi ya makuhani hakuinunua; maana makuhani walikuwa na posho yao kutoka kwa Farao, wakala posho yao waliyopewa na Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ardhi ambayo Yosefu hakuinunua ni ile iliyomilikiwa na makuhani. Hao hawakulazimika kuiuza ardhi yao kwani waliishi kwa posho maalumu waliyopewa na Farao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, hakununua nchi ya makuhani, kwa sababu walikuwa wanapata mgawo wao wa kawaida kutoka kwa Farao, nao walikuwa na chakula cha kuwatosha kutokana na mgawo waliopewa na Farao. Hii ndiyo sababu hawakuuza ardhi yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, hakununua nchi ya makuhani, kwa sababu walikuwa wanapata mgawo wao wa kawaida kutoka kwa Farao, nao walikuwa na chakula cha kuwatosha kutokana na mgawo waliopewa na Farao. Hii ndiyo sababu hawakuuza ardhi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ila nchi ya makuhani hakuinunua; maana makuhani walikuwa na posho yao kutoka kwa Farao, wakala posho yao waliyopewa na Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ardhi ambayo Yosefu hakuinunua ni ile iliyomilikiwa na makuhani. Hao hawakulazimika kuiuza ardhi yao kwani waliishi kwa posho maalumu waliyopewa na Farao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mashamba ya watambikaji tu hakuyanunua, kwani hao watambikaji walikatiwa hayo mashamba na Farao kuwa chakula chao, nao wakajitunza na kuitumia hiyo haki, Farao aliyowapa; kwa sababu hii hawakuyauza mashamba yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ila nchi ya makuhani hakuinunua; maana makuhani walikuwa na posho yao kutoka kwa Farao, wakala posho yao waliyopewa na Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Udongo ambao Yosefu hakununua ni ule iliokuwa wa makuhani. Hao hawakulazimika kuuzisha udongo wao maana waliishi kwa posho waliyopewa na mufalme.