Genesis 47:25 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamjibu, “Bwana, umeyaokoa maisha yetu! Kwa vile umetuonesha wema wako, sisi tutakuwa watumwa wa Farao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamwambia, “Umeokoa maisha yetu. Basi na tupate kibali mbele ya macho ya bwana wetu; tutakuwa watumwa wa Farao.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakasema, Umetulinda hai, na tuone kibali machoni pa bwana wetu, nasi tutakuwa watumwa wa Farao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamjibu, “Bwana, umeyaokoa maisha yetu! Kwa vile umetuonesha wema wako, sisi tutakuwa watumwa wa Farao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamwambia, “Umeokoa maisha yetu. Basi na tupate kibali mbele ya macho ya bwana wetu; tutakuwa watumwa wa Farao.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamwambia, “Umeokoa maisha yetu. Basi na tupate kibali mbele ya macho ya bwana wetu; tutakuwa watumwa wa Farao.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakasema, Umeyaokoa maisha yetu, na tuone kibali machoni pa bwana wetu, nasi tutakuwa watumwa wa Farao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamjibu, “Bwana, umeyaokoa maisha yetu! Kwa vile umetuonesha wema wako, sisi tutakuwa watumwa wa Farao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, waliposema: Umetuponya. Tumeona mapendeleo machoni pa bwana wetu, na tuwe watumwa wake Farao!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakasema, Umetulinda hai, na tuone kibali machoni pa bwana wetu, nasi tutakuwa watumwa wa Farao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamujibu: “Bwana, umeyaokoa maisha yetu! Kwa vile umetuonyesha wema wako, sisi tutakuwa watumwa wa mufalme.”