Genesis 47:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndivyo Yosefu alivyotangaza sheria moja ambayo iko mpaka leo nchini Misri: Kila raia lazima atoe sehemu moja ya tano ya mavuno yake kwa Farao. Ardhi ya makuhani tu ndiyo haikununuliwa na kufanywa mali ya Farao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Yusufu akaiweka iwe sheria ya ardhi katika nchi ya Misri, ambayo inatumika hata leo, kwamba sehemu ya tano ya mazao ni mali ya Farao. Ni ardhi ya makuhani tu ambayo haikuwa ya Farao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yusufu akaifanya sheria kwa habari ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndivyo Yosefu alivyotangaza sheria moja ambayo iko mpaka leo nchini Misri: kila raia lazima atoe sehemu moja ya tano ya mavuno yake kwa Farao. Ardhi ya makuhani tu ndiyo haikununuliwa na kufanywa mali ya Farao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Yosefu akaiweka iwe sheria kuhusu nchi ya Misri, ambayo inatumika mpaka leo, kwamba, sehemu ya tano ya mazao ni mali ya Farao. Ni nchi ya makuhani tu ambayo haikuwa ya Farao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Yusufu akaiweka iwe sheria kuhusu nchi ya Misri, ambayo inatumika mpaka leo, kwamba, sehemu ya tano ya mazao ni mali ya Farao. Ni nchi ya makuhani tu ambayo haikuwa ya Farao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yusufu akaifanya kuwa sheria ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndivyo Yosefu alivyotangaza sheria moja ambayo iko mpaka leo nchini Misri: Kila raia lazima atoe sehemu moja ya tano ya mavuno yake kwa Farao. Ardhi ya makuhani tu ndiyo haikununuliwa na kufanywa mali ya Farao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hayo maongozi, Yosefu aliyoyaweka, yako mpaka siku hii ya leo kwamba: Fungu la tano la mapato ya mashamba ya Misri ni lake Farao. Mashamba yasiyouzwa kuwa yake Farao ni yale ya watambikaji peke yao tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yusufu akaifanya sheria kwa habari ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ndivyo Yosefu alivyotangaza sheria moja ambayo iko mpaka leo katika inchi ya Misri. Kila mwanainchi anapaswa kutoa sehemu moja ya tano ya mavuno yake kwa mufalme. Udongo wa makuhani tu ndio haukununuliwa na kufanywa mali ya mufalme.