Genesis 47:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yakobo akamjibu, “Umri niliojaliwa kama msafiri ni miaka 130. Miaka hiyo imekuwa michache na iliyojaa mateso, tena haijafikia idadi ya miaka waliyoishi wazee wangu kama wasafiri.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Naye Yakobo akamwambia Farao, “Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni miaka mia moja na thelathini. Miaka yangu imekuwa michache na ya taabu, wala haikufikia miaka ya maisha ya baba zangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yakobo akamjibu, “Umri niliojaliwa kama msafiri ni miaka 130. Miaka hiyo imekuwa michache na iliyojaa mateso, tena haijafikia idadi ya miaka waliyoishi wazee wangu kama wasafiri.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Naye Yakobo akamwambia Farao, “Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni miaka 130. Miaka yangu imekuwa michache na ya taabu, wala haikufikia miaka ya kusafiri ya baba zangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Naye Yakobo akamwambia Farao, “Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni miaka 130. Miaka yangu imekuwa michache na ya taabu, wala haikufikia miaka ya kusafiri ya baba zangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yakobo akamjibu Farao, Siku za kuishi kwangu ni miaka mia moja na thelathini; siku za maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikia siku za maisha ya baba zangu katika siku za kuishi kwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yakobo akamjibu, “Umri niliojaliwa kama msafiri ni miaka 130. Miaka hiyo imekuwa michache na iliyojaa mateso, tena haijafikia idadi ya miaka waliyoishi wazee wangu kama wasafiri.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yakobo akamjibu Farao: Siku za miaka ya kukaa huku ugenini ni miaka 130. Siku za miaka ya maisha yangu ni chache, tena ni mbaya, hazikufika kuwa nyingi kama siku za miaka ya kuwapo za baba zangu, walizozikaa huku ugenini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yakobo akamjibu Farao, Siku za miaka ya kusafiri kwangu ni mia na thelathini; siku za miaka ya maisha yangu zimekuwa chache, tena za taabu, wala hazikufikilia siku za miaka ya maisha ya baba zangu katika siku za kusafiri kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yakobo akamujibu: “Umri niliojaliwa kama musafiri ni miaka mia moja na makumi tatu. Miaka hiyo imekuwa michache na iliyojaa mateso, tena haijafikia hesabu ya miaka wazee wangu waliyoishi kama wasafiri.”