Genesis 48:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yosefu akawainua wanawe wawili, Efraimu katika mkono wake wa kulia, akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa baba yake, na Manase katika mkono wake wa kushoto, akimwelekeza kwenye mkono wa kulia wa baba yake, akawasogeza kwa babu yao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yusufu akachukua wale wana wawili, Efraimu kwenye mkono wake wa kuume akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kushoto akimwelekeza kwenye mkono wa kuume wa Israeli, akawaleta karibu na babu yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yusufu akawaweka wote wawili, Efraimu katika mkono wake wa kuume, kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kuume wa Israeli, akawasogeza karibu naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yosefu akawainua wanawe wawili, Efraimu katika mkono wake wa kulia, akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa baba yake, na Manase katika mkono wake wa kushoto, akimwelekeza kwenye mkono wa kulia wa baba yake, akawasogeza kwa babu yao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yosefu akachukua wale wana wawili, Efraimu kwenye mkono wake wa kuume akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kushoto akimwelekeza kwenye mkono wa kuume wa Israeli, akawaleta karibu na babu yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yusufu akachukua wale wana wawili, Efraimu kwenye mkono wake wa kuume akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kushoto akimwelekeza kwenye mkono wa kuume wa Israeli, akawaleta karibu na babu yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yusufu akawaweka wote wawili, Efraimu katika mkono wake wa kulia, kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kulia wa Israeli, akawasogeza karibu naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yosefu akawainua wanawe wawili, Efraimu katika mkono wake wa kulia, akimwelekeza kwenye mkono wa kushoto wa baba yake, na Manase katika mkono wake wa kushoto, akimwelekeza kwenye mkono wa kulia wa baba yake, akawasogeza kwa babu yao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yosefu akawachukua wote wawili, Efuraimu kwa mkono wake wa kuume na kumweka kushotoni kwake Isiraeli, naye Manase kwa mkono wake wa kushoto na kumweka kuumeni kwake Isiraeli; ndivyo, alivyowapeleka kwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yusufu akawaweka wote wawili, Efraimu katika mkono wake wa kuume, kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kuume wa Israeli, akawasogeza karibu naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yosefu akawainua wana wake wawili, Efuraimu katika mukono wake wa kuume, akimwelekeza kwenye mukono wa kushoto wa baba yake, na Manase katika mukono wake wa kushoto, akimwelekeza kwenye mukono wa kuume wa baba yake, akawasogeza kwa babu yao.