Genesis 48:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Naamua hivyo kwa sababu ya mama yako, Raheli. Nilipokuwa narudi kutoka Padani yeye alifariki katika nchi ya Kanaani, tukiwa karibu kufika Efratha, akaniachia huzuni. Basi, nikamzika papo hapo, kando ya njia iendayo Efratha, yaani Bethlehemu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilipokuwa ninarudi kutoka Padani, nilihuzunika sana kwa sababu Raheli alifariki katika nchi ya Kanaani tulipokuwa tukisafiri, tukiwa karibu kufika Efrata. Kwa hiyo nilimzika huko, kando ya njia iendayo Efrata” (yaani Bethlehemu).
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrathi. Nikamzika katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Naamua hivyo kwa sababu ya mama yako, Raheli. Nilipokuwa narudi kutoka Padani yeye alifariki katika nchi ya Kanaani, tukiwa karibu kufika Efratha, akaniachia huzuni. Basi, nikamzika papo hapo, kando ya njia iendayo Efratha, yaani Bethlehemu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilipokuwa ninarudi kutoka Padani, katika huzuni yangu Raheli alifariki katika nchi ya Kanaani tulipokuwa tungali tukisafiri, tukiwa karibu kufika Efrathi. Kwa hiyo nilimzika huko, kando ya njia iendayo Efrathi” (yaani Bethlehemu).
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilipokuwa ninarudi kutoka Padani, katika huzuni yangu Raheli alifariki katika nchi ya Kanaani tulipokuwa tungali tukisafiri, tukiwa karibu kufika Efrathi. Kwa hiyo nilimzika huko, kando ya njia iendayo Efrathi” (yaani Bethlehemu).
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrata. Nikamzika katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Naamua hivyo kwa sababu ya mama yako, Raheli. Nilipokuwa narudi kutoka Padani yeye alifariki katika nchi ya Kanaani, tukiwa karibu kufika Efratha, akaniachia huzuni. Basi, nikamzika papo hapo, kando ya njia iendayo Efratha, yaani Bethlehemu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nilipotoka Mesopotamia nilifiwa na Raheli njiani katika nchi ya Kanaani, uliposalia mwendo wa kipande kifupi tu kufika Efurata, nami nikamzika huko kwenye njia ya kwenda Efurata, ndio Beti-Lehemu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrathi. Nikamzika katika njia ya Efrathi, ndio Bethlehemu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninaamua hivyo kwa sababu ya mama yako, Rakeli. Nilipokuwa ninarudi kutoka Padani yeye alikufa katika inchi ya Kanana, tukiwa karibu kufika Efurata, akaniachia huzuni. Basi, nikamuzika palepale, kando ya njia inayokwenda Efurata, maana yake Betelehemu.”