Genesis 49:25 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia, kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki; upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vilivyo chini, baraka za uzazi wa akina mama na mifugo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za juu mbinguni, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia, kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki; upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vilivyo chini, baraka za uzazi wa akina mama na mifugo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za mbinguni juu, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za mbinguni juu, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naam, kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia; Kwa baraka za juu mbinguni. Baraka za vilindi vilivyo chini, Baraka za maziwa, na za mimba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia, kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki; upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vilivyo chini, baraka za uzazi wa akina mama na mifugo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mungu wa baba yako ndiye atakayekusaidia Mwenyezi Mungu ndiye atakayekubariki kwa mbaraka zitokazo mbinguni juu na kwa mbaraka zitokazo vilindini ndani ya nchi na kwa mbaraka zitokazo maziwani na tumboni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, kwa Mungu wa baba yako atakaye kusaidia; Kwa mibaraka ya mbinguni juu. Mibaraka ya vilindi vilivyo chini, Mibaraka ya maziwa, na ya mimba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu wa baba yako atakusaidia, Mungu Mwenye Nguvu atakubariki, upate baraka za mvua toka juu mbinguni, baraka za maji ya vilindi vinavyokuwa chini, baraka za uzazi wa wamama na nyama.