Genesis 49:29 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha Israeli akawaagiza wanawe hivi, “Mimi karibu nife na kujiunga na watu wangu. Nizikeni pamoja na wazee wangu katika pango lililoko shambani mwa Efroni Mhiti,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha Israeli akawaagiza wanawe hivi, “Mimi karibu nife na kujiunga na watu wangu. Nizikeni pamoja na wazee wangu katika pango lililoko shambani mwa Efroni Mhiti,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo alipowapa maelekezo haya: “Mimi niko karibu kukusanywa kwa watu wangu. Mnizike pamoja na baba zangu kwenye pango katika shamba la Efroni, Mhiti,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango lililomo shambani mwa Efroni, Mhiti;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha Israeli akawaagiza wanawe hivi, “Mimi karibu nife na kujiunga na watu wangu. Nizikeni pamoja na wazee wangu katika pango lililoko shambani mwa Efroni Mhiti,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akawaagiza na kuwaambia: Mimi sasa nitakapochukuliwa kwenda kwao walio ukoo wangu, sharti mnizike kwa baba zangu katika lile pango, lililoko shambani kwake Mhiti Efuroni!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawaamuru, akasema, Mimi ninakwenda kukusanywa pamoja na watu wangu; mnizike pamoja na baba zangu, katika pango iliyomo shambani mwa Efroni, Mhiti;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Israeli akawaagiza wana wake hivi: “Mimi niko karibu kufa na kwenda kukutana na watu wangu. Munizike pamoja na wazee wangu katika pango linalokuwa katika shamba la Efuroni Muhiti,