Genesis 49:30 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
kule Makpela, mashariki ya Mamre, nchini Kanaani. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efroni, Mhiti, liwe lake la kuzikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Ibrahimu alinunua liwe mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
kule Makpela, mashariki ya Mamre, nchini Kanaani. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efroni, Mhiti, liwe lake la kuzikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Abrahamu alinunua kwa ajili ya mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
pango lililoko katika shamba la Makpela, karibu na Mamre huko Kanaani, ambalo Ibrahimu alinunua kwa ajili ya mahali pa kuzikia kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katika lile pango lililomo shambani mwa Makpela, lililo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, alilolinunua Abrahamu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
kule Makpela, mashariki ya Mamre, nchini Kanaani. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efroni, Mhiti, liwe lake la kuzikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndilo pango lile lililoko shambani kwa Makipela kuelekea Mamure; shamba hilo Aburahamu alilinunua kwa Mhiti Efuroni kuwa mahali pake yeye pa kuzikia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika ile pango iliyomo shambani mwa Makpela, iliyo mbele ya Mamre katika nchi ya Kanaani, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kule Makipela, upande wa mashariki wa Mamure, katika inchi ya Kanana. Abrahamu alinunua pango na shamba hilo kwa Efuroni, Muhiti, likuwe lake la kuzikia.