Genesis 49:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
lakini mimi sitashiriki njama zao; ee roho yangu, usishiriki mikutano yao, maana, katika hasira yao, walimuua mtu, kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, na kukata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
lakini mimi sitashiriki njama zao; ee roho yangu, usishiriki mikutano yao, maana, katika hasira yao, walimuua mtu, kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, walikata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mimi na nisiingie katika baraza lao, nami nisiunganike katika kusanyiko lao, kwa kuwa wamewaua watu katika hasira yao, walikata mishipa ya miguu ya mafahali kama walivyopenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimwua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng'ombe;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
lakini mimi sitashiriki njama zao; ee roho yangu, usishiriki mikutano yao, maana, katika hasira yao, walimuua mtu, kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Roho yangu isiingie penye njama yao, wala moyo wangu usifanye bia na mikutano yao! Kwani kwa makali yao waliua watu, kwa majivuno yao wakakata madume ya ng'ombe mishipa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nafsi yangu, usiingie katika siri yao, Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao, Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu, Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng’ombe;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
lakini mimi sitashiriki mashauri yao mabaya. Ee roho yangu, usishiriki mikutano yao, maana, katika hasira yao, walimwua mutu, kwa mapenzi yao walikata mushipa wa ngombe.