Genesis 5:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alimwita mtoto huyo Noa, akisema, “Mtoto huyu ndiye atakayetufariji kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika ardhi aliyoilaani Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akamwita jina Nuhu. Naye akasema, “Huyu ndiye atakayetufariji katika kazi ngumu ya mikono yetu yenye maumivu makali yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Mwenyezi Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alimwita mtoto huyo Noa, akisema, “Mtoto huyu ndiye atakayetufariji kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika ardhi aliyoilaani Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na BWANA.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akamwita jina lake Nuhu, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na bwana.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alimwita mtoto huyo Noa, akisema, “Mtoto huyu ndiye atakayetufariji kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika ardhi aliyoilaani Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akamwita jinala lake Noa (Tulia) kwa kwamba: Huyu ndiye atakayetutuliza mioyo kwa ajili ya kazi zetu, mikono yetu inazozifanya kwa uchungu katika nchi, aliyoiapiza Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwita jina lake Nuhu, akinena, Huyu ndiye atakayetufariji kwa kazi yetu na kwa taabu ya mikono yetu katika nchi aliyoilaani BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akamwita mutoto yule Noa, akisema: “Mutoto huyu ndiye atakayetufariji kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika inchi ambayo Yawe alilaani.”