Genesis 50:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walipofika katika uwanja wa kupuria nafaka wa Atadi, ngambo ya mto Yordani, waliomboleza kwa huzuni kubwa, naye Yosefu akamfanyia baba yake marehemu matanga ya siku saba.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipofika kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Atadi, karibu na Yordani, wakalia kwa sauti na kwa uchungu. Yusufu akakaa huko kwa siku saba kumwombolezea baba yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaja mpaka sakafu ya Atadi, iliyo ng'ambo ya Yordani. Wakaomboleza huko maombolezo makuu, mazito sana. Akafanya matanga ya babaye siku saba.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Walipofika katika uwanja wa kupuria nafaka wa Atadi, ng'ambo ya mto Yordani, waliomboleza kwa huzuni kubwa, naye Yosefu akamfanyia baba yake marehemu matanga ya siku saba.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipofika kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Atadi, karibu na Yordani, wakalia kwa sauti na kwa uchungu; Yosefu akapumzika huko kwa siku saba kumwombolezea baba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipofika kwenye sakafu ya kupuria nafaka ya Atadi, karibu na Yordani, wakalia kwa sauti na kwa uchungu; Yusufu akapumzika huko kwa siku saba kumwombolezea baba yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaja mpaka uwanja wa kupuria nafaka wa Atadi, uliyo ng'ambo ya Yordani. Wakaomboleza huko maombolezo makuu, mazito sana. Akafanya matanga ya baba yake siku saba.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walipofika katika uwanja wa kupuria nafaka wa Atadi, ngambo ya mto Yordani, waliomboleza kwa huzuni kubwa, naye Yosefu akamfanyia baba yake marehemu matanga ya siku saba.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Walipofika pake Atadi pa kupuria ngano palipo ng'ambo ya huko ya Yordani wakafanya maombolezo makuu yenye vilio kabisa. Ndivyo, Yosefu alivyolala matanga siku saba kwa ajili ya baba yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaja mpaka sakafu ya Atadi, iliyo ng’ambo ya Yordani. Wakaomboleza huko maombolezo makuu, mazito sana. Akafanya matanga ya babaye siku saba.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Walipofika katika uwanja wa kupepetea ngano wa Atadi, ngambo ya muto Yordani, waliomboleza kwa huzuni kubwa, naye Yosefu akamufanyia baba yake marehemu kilio cha siku saba.