Genesis 50:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Walimchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika katika pango lililokuwa katika shamba kule Makpela, mashariki ya Mamre. Pango pamoja na shamba hilo Abrahamu alikuwa amelinunua kwa Efroni Mhiti, ili pawe mahali pake pa kuzikia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamchukua hadi nchi ya Kanaani, wakamzika kwenye pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre, ambalo Ibrahimu alilinunua kutoka kwa Efroni Mhiti pamoja na shamba liwe mahali pa kuzikia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kwa kuwa wanawe wakamchukuwa mpaka nchi ya Kanaani, nao wakamzika katika pango ya shamba la Makpela, iliyo mbele ya Mamre, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake pa kuzikia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
walimchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika katika pango lililokuwa katika shamba kule Makpela, mashariki ya Mamre. Pango pamoja na shamba hilo Abrahamu alikuwa amelinunua kwa Efroni Mhiti, ili pawe mahali pake pa kuzikia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika kwenye pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre, ambalo Abrahamu alilinunua kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba liwe mahali pa kuzikia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika kwenye pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre, ambalo Ibrahimu alilinunua kutoka kwa Efroni, Mhiti, pamoja na shamba liwe mahali pa kuzikia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kwa kuwa wanawe wakamchukua mpaka nchi ya Kanaani, na wakamzika katika pango la shamba la Makpela, lililo mbele ya Mamre, alilonunua Abrahamu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake ya kuzikia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Walimchukua mpaka nchi ya Kanaani, wakamzika katika pango lililokuwa katika shamba kule Makpela, mashariki ya Mamre. Pango pamoja na shamba hilo Abrahamu alikuwa amelinunua kwa Efroni Mhiti, ili pawe mahali pake pa kuzikia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wao wanawe wakamchkua na kumpeleka katika nchi ya Kanaani, kisha wakamzika katika lile pango katika shamba la Makipela, ndilo shamba lile, Aburahamu alilolinunua kwa Mhiti Efuroni kuwa mahali pake pa kuzikia, napo palikuwa panaelekea Mamure.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kwa kuwa wanawe wakamchukuwa mpaka nchi ya Kanaani, nao wakamzika katika pango ya shamba la Makpela, iliyo mbele ya Mamre, aliyoinunua Ibrahimu pamoja na shamba kwa Efroni Mhiti, pawe milki yake pa kuzikia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
wakamupeleka mpaka inchi ya Kanana, wakamuzika katika pango lililokuwa katika shamba kule Makipela, upande wa mashariki wa Mamure. Pango pamoja na shamba lile Abrahamu alikuwa amelinunua kwa Efuroni Muhiti, kusudi pakuwe pahali pake pa kuzikia.