Genesis 50:24 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baadaye Yosefu aliwaambia ndugu zake, “Mimi sasa ninakaribia kufa. Lakini Mungu hakika atawajia kuwasaidia. Atawatoa katika nchi hii na kuwapelekeni katika nchi aliyowaapia Abrahamu, Isaka na Yakobo.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Yusufu akawaambia ndugu zake, “Mimi ninakaribia kufa. Lakini kwa hakika Mungu atawasaidia na kuwachukueni kutoka nchi hii na kuwapeleka katika nchi aliyomwahidi kwa kiapo Ibrahimu, Isaka na Yakobo.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baadaye Yosefu aliwaambia ndugu zake, “Mimi sasa ninakaribia kufa. Lakini Mungu hakika atawajia kuwasaidia. Atawatoa katika nchi hii na kuwapelekeni katika nchi aliyowaapia Abrahamu, Isaka na Yakobo.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo Yosefu akawaambia ndugu zake, “Mimi ninakaribia kufa. Lakini kwa hakika Mungu atawasaidia na kuwachukueni kutoka nchi hii na kuwapeleka katika nchi aliyomwahidi kwa kiapo Abrahamu, Isaki na Yakobo.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo Yusufu akawaambia ndugu zake, “Mimi ninakaribia kufa. Lakini kwa hakika Mungu atawasaidia na kuwachukueni kutoka nchi hii na kuwapeleka katika nchi aliyomwahidi kwa kiapo Ibrahimu, Isaka na Yakobo.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yusufu akawaambia ndugu zake, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baadaye Yosefu aliwaambia ndugu zake, “Mimi sasa ninakaribia kufa. Lakini Mungu hakika atawajia kuwasaidia. Atawatoa katika nchi hii na kuwapelekeni katika nchi aliyowaapia Abrahamu, Isaka na Yakobo.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Yosefu akawaambia ndugu zake: Mimi ninakufa, lakini ninyi Mungu atawapatia njia ya kuwatoa katika nchi hii na kuwapandisha kwenda katika hiyo nchi, aliyowaapia akina Aburahamu na Isaka na Yakobo kuwapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yusufu akawaambia nduguze, Mimi ninakufa, lakini Mungu atawajia ninyi bila shaka, atawapandisha toka nchi hii, mpaka nchi aliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha Yosefu akawaambia wandugu zake: “Mimi sasa ninakaribia kufa. Lakini Mungu hakika atawafikia kwa kuwasaidia. Atawatoa katika inchi hii na kuwapeleka katika inchi aliyowaapia Abrahamu, Isaka na Yakobo.”