Genesis 6:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu akamwambia Noa, “Nimeamua kuwaangamiza binadamu wote kwa sababu wameijaza dunia ukatili. Naam, nitawaangamiza kabisa pamoja na dunia!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Mungu akamwambia Nuhu, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika nitaangamiza watu pamoja na dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu akamwambia Noa, “Nimeamua kuwaangamiza binadamu wote kwa sababu wameijaza dunia ukatili. Naam, nitawaangamiza kabisa pamoja na dunia!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa jeuri kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Mungu akamwambia Nuhu, “Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila kiumbe umefika mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia maovu, basi nitawaangamiza pamoja na dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu akamwambia Noa, “Nimeamua kuwaangamiza binadamu wote kwa sababu wameijaza dunia ukatili. Naam, nitawaangamiza kabisa pamoja na dunia!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Mungu alipomwambia Noa: Mwisho wao wote wenye miili umefika machoni pangu, kwani wameijaza nchi makorofi yao, kwa hiyo wataniona, nikiwaangamiza pamoja na nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu akamwambia Noa: “Nimeamua kuwaangamiza wanadamu wote kwa sababu wamejaza dunia mateso makali. Hakika, nitawaangamiza kabisa pamoja na dunia!