Genesis 6:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitaleta gharika ili kuangamiza viumbe vyote hai duniani. Kila kiumbe hai duniani kitakufa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitaleta gharika ya maji juu ya dunia ili kuangamiza kila chenye uhai chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya dunia kitaangamia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitaleta gharika ili kuangamiza viumbe vyote hai duniani. Kila kiumbe hai duniani kitakufa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitaleta gharika ya maji juu ya nchi ili kuangamiza uhai wote chini ya mbingu, kila kiumbe chenye pumzi ya uhai ndani yake. Kila kitu juu ya nchi kitaangamia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitaleta gharika ili kuangamiza viumbe vyote hai duniani. Kila kiumbe hai duniani kitakufa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani tazama: Mimi nitaleta mafuriko ya maji juu ya nchi, niwaangamize wote wenye miili walio na pumzi za uzima, walioko chini ya mbingu; wote pia wanaokaa katika nchi sharti wafe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, nitaleta gharika ya maji juu ya nchi, niharibu kila kitu chenye mwili na pumzi ya uhai, kisiwepo chini ya mbingu; kila kilichoko duniani kitakufa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitaleta mafuriko ya maji kwa kuangamiza viumbe vyote vyenye uzima katika dunia. Kila kiumbe chenye uzima katika dunia kitakufa.