Genesis 6:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Mwenyezi-Mungu akasema, “Roho yangu haitakaa ndani ya binadamu milele, maana yeye ni wa kufa tu. Basi, hataishi zaidi ya miaka 120.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo Mwenyezi Mungu akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa; siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Mwenyezi-Mungu akasema, “Roho yangu haitakaa ndani ya binadamu milele, maana yeye ni wa kufa tu. Basi, hataishi zaidi ya miaka 120.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo BWANA akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo bwana akasema, “Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye ni wa kufa, siku zake zitakuwa miaka 120.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mwili; basi siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Mwenyezi-Mungu akasema, “Roho yangu haitakaa ndani ya binadamu milele, maana yeye ni wa kufa tu. Basi, hataishi zaidi ya miaka 120.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Bwana aliposema: Roho yangu haiwezi kubishana na watu kale na kale, kwani kwa hivyo, walivyopotea, mioyo yao imegeuka kuwa nyama tupu. Basi, siku zao na ziwe bado miaka 120.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni nyama; basi siku zake zitakuwa miaka mia na ishirini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Yawe akasema: “Roho yangu haitakaa ndani ya wanadamu milele, maana yeye ni wa kufa tu. Basi, hataishi zaidi ya miaka mia moja na makumi mbili.”