Genesis 6:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyakati hizo na hata baadaye, kulikuwa na majitu duniani ambao walikuwa wazawa wa watoto wa kiume wa Mungu na wasichana wa watu. Hao ndio watu waliokuwa mashujaa na wenye sifa enzi hizo, nao waliitwa Wanefili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanefili walikuwa duniani siku hizo, na hata baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa wa zamani, na watu mashuhuri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao Wanefili?b
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyakati hizo na hata baadaye, kulikuwa na majitu duniani ambao walikuwa wazawa wa watoto wa kiume wa Mungu na wasichana wa watu. Hao ndio watu waliokuwa mashujaa na wenye sifa enzi hizo, nao waliitwa Wanefili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanefili walikuwako duniani siku hizo, na baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa hao binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanefili walikuwako duniani siku hizo, na baadaye, hao wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu na kuzaa nao. Wanefili walikuwa mashujaa na watu waliojulikana wa zamani hizo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyakati hizo na hata baadaye, kulikuwa na majitu duniani ambao walikuwa wazawa wa watoto wa kiume wa Mungu na wasichana wa watu. Hao ndio watu waliokuwa mashujaa na wenye sifa enzi hizo, nao waliitwa Wanefili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile walikuwako katika nchi nao watu walio majitu; hata baadaye siku zote wana wa Mungu walipoingia kwao wana wa kike na watu, nao waliwazalia wana; hawa ndio wale wenye nguvu waliojipatia jina kuu tangu kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku zile na hata kisha, kulikuwa majitu katika dunia ambao walikuwa wazao wa wana wa Mungu na wabinti za wanadamu. Hao ndio watu waliokuwa mashujaa na wenye sifa wa zamani, na waliitwa Wanefili.