Genesis 7:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa hai duniani: Binadamu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Vyote viliangamizwa duniani. Noa tu ndiye aliyesalimika na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali; watu, wanyama pori, viumbe vinavyotambaa ardhini, na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Nuhu peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa hai duniani: binadamu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Vyote viliangamizwa duniani. Noa tu ndiye aliyesalimika na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Nuhu peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kila kilichokuwa hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali; mwanadamu, wanyama wa kufugwa, kitambaacho na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao waliokuwa pamoja naye katika safina.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa hai duniani: Binadamu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Vyote viliangamizwa duniani. Noa tu ndiye aliyesalimika na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, alivyowatowesha wote waliosimama juu ya nchi kuanzia watu, tena nyama na wadudu nao ndege wa angani, walitoweshwa wote katika nchi, akasalia Noa peke yake pamoja nao waliokuwa naye mle chomboni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa na pumzi ya uzima katika dunia: wanadamu, nyama, viumbe vinavyotambaa na ndege wa anga. Vyote viliangamizwa katika dunia. Noa tu ndiye aliyebaki na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya chombo.