Genesis 7:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya siku saba, nitanyesha mvua nchini siku arubaini mchana na usiku, na kila kiumbe hai nilichokiumba duniani nitakiangamiza.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya dunia kwa siku arobaini, usiku na mchana; nami nitafutilia mbali kutoka uso wa dunia kila kiumbe hai nilichokiumba.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya siku saba, nitanyesha mvua nchini siku arubaini mchana na usiku, na kila kiumbe hai nilichokiumba duniani nitakiangamiza.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Siku saba tangu sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini mchana na usiku, nami nitafutilia mbali kutoka katika uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini usiku na mchana, nami nitafutilia mbali kutoka uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya siku saba, nitanyesha mvua nchini siku arubaini mchana na usiku, na kila kiumbe hai nilichokiumba duniani nitakiangamiza.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ziko bado siku saba, ndipo, mimi nitakaponyesha mvua siku 40 mchana kutwa na usiku kucha, niwatoweshe katika nchi yote nzima wote pia wanaosimama bado, niliowaumba mimi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arobaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya siku saba, nitanyesha mvua juu ya inchi siku makumi ine muchana na usiku, na kila kiumbe chenye uzima nilichokiumba katika dunia nitakiangamiza.”