Genesis 8:11 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Njiwa huyo akamrudia Noa saa za jioni akiwa na tawi bichi la mzeituni mdomoni mwake. Kwa hiyo Noa akajua kwamba maji yalikuwa yamepungua katika nchi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Jioni hua aliporudi kwa Nuhu alikuwa amebeba jani bichi la mzeituni lililochumwa wakati ule ule katika mdomo wake! Ndipo Nuhu akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Njiwa huyo akamrudia Noa saa za jioni akiwa na tawi bichi la mzeituni mdomoni mwake. Kwa hiyo Noa akajua kwamba maji yalikuwa yamepungua katika nchi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati hua aliporejea kwa Noa jioni, alikuwa amechukua katika mdomo wake jani bichi la mzeituni, lililochumwa wakati ule ule! Ndipo Noa akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya uso wa dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati hua aliporejea kwa Nuhu jioni, alikuwa amechukua katika mdomo wake jani bichi la mzeituni, lililochumwa wakati ule ule! Ndipo Nuhu akajua ya kuwa maji yameondoka juu ya uso wa dunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelichuma, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Njiwa huyo akamrudia Noa saa za jioni akiwa na tawi bichi la mzeituni mdomoni mwake. Kwa hiyo Noa akajua kwamba maji yalikuwa yamepungua katika nchi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu njiwa aliporudi kwake saa za jioni, akaona mdomoni mwake jani la mchekele, alilolivunja. Ndipo, Noa alipotambua, ya kuwa maji yamepunguaka katika nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelitunda, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Njiwa yule akamurudilia Noa saa za magaribi akiwa na tawi bichi la muzeituni katika midomo yake. Kwa hiyo Noa akajua kwamba maji yalikuwa yamepunguka katika inchi.