Genesis 8:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Noa alipokuwa na umri wa miaka 601, siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Noa akafunua kifuniko cha safina na alipotazama, akaona kwamba nchi ilikuwa imekauka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kufikia siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza wa mwaka wa mia sita na moja (601) wa maisha ya Nuhu, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Nuhu akatoa kifuniko juu ya safina, akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Noa alipokuwa na umri wa miaka 601, siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Noa akafunua kifuniko cha safina na alipotazama, akaona kwamba nchi ilikuwa imekauka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka 601, wa kuishi kwake Noa, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Noa akafungua mlango wa safina akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka 601, wa kuishi kwake Nuhu, maji yalikuwa yamekauka duniani. Kisha Nuhu akafungua mlango wa safina akaona ya kuwa uso wa ardhi ulikuwa umekauka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Noa alipokuwa na umri wa miaka 601, siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Noa akafunua kifuniko cha safina na alipotazama, akaona kwamba nchi ilikuwa imekauka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ikawa katika mwaka wa 601 katika mwezi wa kwanza siku ya kwanza ya mwezi, ndipo, maji yalipokauka na kutoweka juu ya nchi. Naye Noa alipokiondoa kipaa cha chombo kutazama, akaona, ya kuwa nchi imekauka juu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ikawa mwaka wa mia sita na moja, mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikauka juu ya nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, naye akaona, na tazama, uso wa nchi umekauka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Noa alipokuwa na umri wa miaka mia sita na moja, siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, maji yalikuwa yamekauka katika inchi. Noa akafunua kifuniko cha chombo, na alipoangalia, akaona kwamba inchi ilikuwa imekauka.