Genesis 8:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Toa pia viumbe wote hai wa kila aina waliokuwa pamoja nawe, ndege na wanyama na kila kiumbe kitambaacho, wapate kuzaa kwa wingi duniani, waongezeke na kuenea kila mahali duniani.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe, wakiwamo ndege, wanyama na viumbe vyote vinavyotambaa ardhini, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Toa pia viumbe wote hai wa kila aina waliokuwa pamoja nawe, ndege na wanyama na kila kiumbe kitambaacho, wapate kuzaa kwa wingi duniani, waongezeke na kuenea kila mahali duniani.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utoe nje kila aina ya kiumbe hai aliye pamoja nawe: Ndege, wanyama na viumbe vyote vitambaavyo juu ya ardhi, ili wakazae, na kuongezeka na kuijaza tena dunia.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Toa pia viumbe wote hai wa kila aina waliokuwa pamoja nawe, ndege na wanyama na kila kiumbe kitambaacho, wapate kuzaa kwa wingi duniani, waongezeke na kuenea kila mahali duniani.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao nyama wote walioko kwako, wao wote wenye miili: ndege na nyama na wadudu wote waliotambaa katika nchi watoe pamoja na wewe, wajiendee po pote katika nchi, wapate kuzaa na kuwa wengi tena katika nchi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ondoa vilevile viumbe vyote vyenye uzima vya kila aina vilivyokuwa pamoja nawe, ndege na nyama na kila kiumbe kinachotambaa, vipate kuzaa kwa wingi katika dunia, viongezeke na kuenea kila pahali katika dunia.”