Genesis 8:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Noa akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu, akatwaa mmoja katika kila aina ya wanyama walio safi na ndege walio safi, akamtolea Mungu sadaka za kuteketezwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Nuhu akamjengea Mwenyezi Mungu madhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama na ndege wote walio safi, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nuhu akamjengea Bwana madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Noa akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu, akatwaa mmoja katika kila aina ya wanyama walio safi na ndege walio safi, akamtolea Mungu sadaka za kuteketezwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Noa akamjengea BWANA madhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama wote wasio najisi na ndege wasio najisi, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Nuhu akamjengea bwana madhabahu, akachukua baadhi ya wale wanyama na ndege wote walio safi, akatoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Noa akamjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu, akatwaa mmoja katika kila aina ya wanyama walio safi na ndege walio safi, akamtolea Mungu sadaka za kuteketezwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Noa akamjengea Bwana pa kumtambikia, akatoa wengine katika nyama wote wa nyumbani wanaotakata na katika ndege wote wanaotakata, akawatolea hapo pa kumtambikia Bwana kuwa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nuhu akamjengea BWANA madhabahu; akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi, akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Noa akamujengea Yawe mazabahu, akatwaa mumoja katika kila aina ya nyama wanaohesabiwa kuwa safi na ndege anayehesabiwa kuwa safi, akamutolea Mungu sadaka za kuteketezwa kwa moto juu ya mazabahu.