Habakkuk 1:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanawadhihaki wafalme, na kuwadharau watawala. Kila ngome kwao ni mzaha, wanairundikia udongo na kuiteka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanawabeza wafalme, na kuwadhihaki watawala. Wanaicheka miji yote yenye ngome; wanalundika udongo na kuiteka hiyo miji.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana hufanya chungu ya mavumbi, na kuitwaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanawadhihaki wafalme, na kuwadharau watawala. Kila ngome kwao ni mzaha, wanairundikia udongo na kuiteka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanawabeza wafalme na kuwadhihaki watawala. Wanaicheka miji yote, iliyozungushiwa maboma; wanafanya malundo ya udongo na kuiteka hiyo miji.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanawabeza wafalme, na kuwadhihaki watawala. Wanaicheka miji yote iliyozungushiwa maboma; wanafanya malundo ya udongo na kuiteka hiyo miji.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana huirundikia udongo, na kuitwaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanawadhihaki wafalme, na kuwadharau watawala. Kila ngome kwao ni mzaha, wanairundikia udongo na kuiteka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hao ndio watakaowafyoza wafalme, hata wakuu watawacheka; hao ndio watakaoteka kila boma, maana hulikusanyia mchanga kuwa boma, kisha huliteka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naam, huwadhihaki wafalme, na wakuu ni kitu cha kudharauliwa kwake; huidharau kila ngome; kwa maana hufanya chungu ya mavumbi, na kuitwaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanawachekelea wafalme, na kuwazarau watawala. Kila kuta kwao ni muzaha, wanailundikia udongo na kuiteka.