Habakkuk 1:12 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Je, wewe si ndiwe Mwenyezi-Mungu, tangu kale na kale? Wewe ndiwe Mungu wangu, Mtakatifu wangu, usiyekufa Ee Mwenyezi-Mungu, umewateua Wakaldayo watuhukumu; Ewe Mwamba, umewaimarisha ili watuadhibu!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mwenyezi Mungu, je, wewe sio wa tangu milele? Mungu wangu, Uliye Mtakatifu wangu, hatutakufa. Ee Mwenyezi Mungu, umewachagua wao ili watekeleze hukumu; Ee Mwamba, umewaamuru watuadhibu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee Bwana, umemwandikia hukumu, nawe, Ee Jabali, umemweka imara ili aadhibishwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Je, wewe si ndiwe Mwenyezi-Mungu, tangu kale na kale? Wewe ndiwe Mungu wangu, Mtakatifu wangu, usiyekufa Ee Mwenyezi-Mungu, umewateua Wakaldayo watuhukumu; Ewe Mwamba, umewaimarisha ili watuadhibu!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee BWANA, je, wewe sio wa tangu milele? Mungu wangu, Mtakatifu wangu, hatutakufa. Ee BWANA, umewachagua wao ili watekeleze hukumu; Ee Mwamba, umewaamuru watuadhibu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee bwana, je, wewe sio wa tangu milele? Mungu wangu, Uliye Mtakatifu wangu, hatutakufa. Ee bwana, umewachagua wao ili watekeleze hukumu; Ee Mwamba, umewaamuru watuadhibu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee BWANA, umemwandikia hukumu, nawe, Ee Jabali, umemweka imara ili aadhibishwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Je, wewe si ndiwe Mwenyezi-Mungu, tangu kale na kale? Wewe ndiwe Mungu wangu, Mtakatifu wangu, usiyekufa Ee Mwenyezi-Mungu, umewateua Wakaldayo watuhukumu; Ewe Mwamba, umewaimarisha ili watuadhibu!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kumbe wewe Bwana, siwe Mungu wangu mtakatifu toka kale? Kwa hiyo hatutakufa. Wewe Bwana, umemweka, atupatilize; wewe Mwamba wetu, umemtia nguvu, atuchapue.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee BWANA, umemwandikia hukumu, nawe, Ee Jabali, umemweka imara ili aadhibishwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe si ndiwe Yawe, tangu zamani sana? Wewe ndiwe Mungu wangu, Mutakatifu wangu, usiyekufa. Ee Yawe, umewachagua Wakaldea watuhukumu! Ewe kimbilio letu, umewaimarisha kusudi watuazibu!