Habakkuk 1:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wewe ni mtakatifu kabisa, huwezi kutazama uovu, huwezi kustahimili kamwe kuona mabaya. Mbona basi wawaona wafanya maovu na kunyamaza, kwa nini unanyamaza waovu wanapowamaliza wale watu walio waadilifu kuliko wao?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Macho yako ni safi mno hata yasiweze kuutazama uovu, wala huwezi kuvumilia makosa. Kwa nini basi unawavumilia wadanganyifu? Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu wanawameza wale wenye haki kuliko wao wenyewe?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wewe ni mtakatifu kabisa, huwezi kutazama uovu, huwezi kustahimili kamwe kuona mabaya. Mbona basi wawaona wafanya maovu na kunyamaza, kwa nini unanyamaza waovu wanapowamaliza wale watu walio waadilifu kuliko wao?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Macho yako ni safi mno hata yasiweze kutazama uovu, wala huwezi kuvumilia makosa. Kwa nini basi unawavumilia wadanganyifu? Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu wakiwameza wale wenye haki kuliko wao wenyewe?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Macho yako ni safi mno hata yasiweze kuutazama uovu, wala huwezi kuvumilia makosa. Kwa nini basi unawavumilia wadanganyifu? Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu wanawameza wale wenye haki kuliko wao wenyewe?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wewe ni mtakatifu kabisa, huwezi kutazama uovu, huwezi kustahimili kamwe kuona mabaya. Mbona basi wawaona wafanya maovu na kunyamaza, kwa nini unanyamaza waovu wanapowamaliza wale watu walio waadilifu kuliko wao?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Macho yako yanatakata, hayawezi kuyaona tu hayo mabaya, huwezi kabisa kuvitazama tu, watu wanavyosumbuliwa. Mbona sasa unawatazama tu wapokonyaji na kujinyamazia kimya, asiyekucha akimmeza aliye mwongofu kuliko yeye?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wewe ni mutakatifu kabisa, hauwezi kutazama uovu, hauwezi kuvumilia hata kidogo kuona mabaya. Mbona basi unawaona wafanya maovu na kunyamaza, kwa nini unanyamaza waovu wanapowamaliza wale watu wanaokuwa wenye haki kuliko wao?