Habakkuk 1:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana ninawachochea Wakaldayo, taifa lile kali na lenye hamaki! Taifa lipitalo katika nchi yote, ili kunyakua makao ya watu wengine.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama! Nitawainua Wakaldayo, watu wakatili na wenye haraka, ambao hupita dunia yote ili kuteka makazi yasiyo yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana, angalieni, nawaondokesha Wakaldayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana ninawachochea Wakaldayo, taifa lile kali na lenye hamaki! Taifa lipitalo katika nchi yote, ili kunyakua makao ya watu wengine.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitawainua Wababeli, watu hao wakatili na wenye haraka, ambao hupita dunia yote kuteka mahali pa kuishi pasipo pao wenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitawainua Wakaldayo, watu hao wakatili na wenye haraka, ambao hupita dunia yote kuteka mahali pa kuishi pasipo pao wenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana, angalieni, nawachochea Wakaldayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana ninawachochea Wakaldayo, taifa lile kali na lenye hamaki! Taifa lipitalo katika nchi yote, ili kunyakua makao ya watu wengine.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mtaniona, nikiwainua Wakasidi, lile taifa kali lenye mioyo miepesi, ni wale wanaokwenda katika nchi za mbali, wajipatie makao yasiyo yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana, angalieni, nawaondokesha Wakaldayo, taifa lile kali, lenye haraka kupita kiasi; wapitao katikati ya dunia, ili wayamiliki makao yasiyo yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana ninawachochea Wakaldea, taifa lile kali na lenye nguvu, taifa linalopita katika inchi yote, kwa kunyanganya makao ya watu wengine.