Habakkuk 1:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wote wanakuja kufanya ukatili; kwa nyuso kakamavu wanasonga mbele, wanakusanya mateka wengi kama mchanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wote wanakuja tayari kutenda udhalimu. Makundi yao wanasonga mbele kama upepo wa jangwani, na kukusanya wafungwa kama mchanga.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Waja wote ili kufanya udhalimu; nyuso zao zimeelekezwa kwa bidii yao kama upepo wa mashariki, nao hukusanya mateka kama mchanga.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wote wanakuja kufanya ukatili; kwa nyuso kakamavu wanasonga mbele, wanakusanya mateka wengi kama mchanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wote wanakuja tayari kwa fujo. Makundi yao ya wajeuri yanasonga mbele kama upepo wa jangwani na kukusanya wafungwa kama mchanga.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wote wanakuja tayari kwa fujo. Makundi yao ya wajeuri yanasonga mbele kama upepo wa jangwani, na kukusanya wafungwa kama mchanga.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanakuja wote ili kufanya udhalimu; nyuso zao zimeelekezwa kwa bidii yao kama upepo wa mashariki, nao hukusanya mateka kama mchanga.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wote wanakuja kufanya ukatili; kwa nyuso kakamavu wanasonga mbele, wanakusanya mateka wengi kama mchanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao wote hujia kukorofisha, nyuso zao zote pia zikiwa zimeelekea mbele, hukusanya mateka kama ni mchanga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Waja wote ili kufanya udhalimu; nyuso zao zimeelekezwa kwa bidii yao kama upepo wa mashariki, nao hukusanya mateka kama mchanga.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wote wanakuja kwa kutesa kwa ukali; wanafukuzia wakikaza macho mbele, wanakusanya wafungwa wengi kama muchanga.