Habakkuk 2:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ole wako unayewalewesha jirani zako, na kutia sumu katika divai yao ili upate kuwaona wamekaa uchi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ole wake yeye awapaye majirani zake kileo, akikimimina kutoka kwa kiriba cha mvinyo hadi wamelewa, ili apate kutazama miili yao iliyo uchi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ole wako unayewalewesha jirani zako, na kutia sumu katika divai yao ili upate kuwaona wamekaa uchi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, akiimimina kutoka kwenye kiriba cha mvinyo mpaka wamelewa, ili apate kutazama miili yao iliyo uchi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Ole wake yeye awapaye jirani zake kileo, akiimimina kutoka kwenye kiriba cha mvinyo mpaka wamelewa, ili apate kutazama miili yao iliyo uchi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ole wako unayewalewesha jirani zako, na kutia sumu katika divai yao ili upate kuwaona wamekaa uchi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yatampata amnyweshaye mwenziwe kinywaji, alichokichanganya na makali yake! Kisha anamlewesha, kusudi auone uchi wake na kumfurahia!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole wako unayewalewesha jirani zako, na kutia sumu katika divai yao kusudi upate kuwaona wakiikaa uchi.