Habakkuk 2:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utajaa aibu badala ya heshima. Utakunywa wewe mwenyewe na kupepesuka! Mwenyezi-Mungu mwenyewe atakulevya, na aibu itaifunika heshima yako!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utajazwa na aibu badala ya utukufu. Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue! Kikombe kutoka mkono wa kuume wa Mwenyezi Mungu kinakujia, na aibu itafunika utukufu wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kuume wa Bwana kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utajaa aibu badala ya heshima. Utakunywa wewe mwenyewe na kupepesuka! Mwenyezi-Mungu mwenyewe atakulevya, na aibu itaifunika heshima yako!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utajazwa na aibu badala ya utukufu. Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue! Kikombe kutoka kwenye mkono wa kuume wa BWANA kinakujia, na aibu itafunika utukufu wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utajazwa na aibu badala ya utukufu. Sasa ni zamu yako! Kunywa na ujifunue! Kikombe kutoka kwenye mkono wa kuume wa bwana kinakujia, na aibu itafunika utukufu wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kulia wa BWANA kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utajaa aibu badala ya heshima. Utakunywa wewe mwenyewe na kupepesuka! Mwenyezi-Mungu mwenyewe atakulevya, na aibu itaifunika heshima yako!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Umejishibisha yatiayo soni ukiyaacha yenye utukufu, lakini wewe nawe sharti unywe, ujulikane kuwa mtu asiyetahiriwa. Kikombe kilichomo kuumeni mwa Bwana kinakufikia, utukufu wako ufunikwe nayo yenye soni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Umejaa aibu badala ya utukufu; unywe nawe, uwe kama mtu asiyetahiriwa; kikombe cha mkono wa kuume wa BWANA kitageuzwa ukipokee, na aibu kuu itakuwa juu ya utukufu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utajaa haya pahali pa heshima. Utakunywa wewe mwenyewe na kupepesuka! Yawe mwenyewe atakulewesha, na haya itaifunika heshima yako!