Habakkuk 2:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maovu uliyoitenda Lebanoni yatakuvamia wewe; uliwaua wanyama, wanyama nao watakutisha. Yote hayo yatakupata wewe, kwa mauaji na dhuluma uliyoitendea dunia, naam, uliyoifanyia miji na wakazi wake wote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika, na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha. Kwa sababu umemwaga damu ya mtu; umeharibu nchi na miji na kila mmoja aliye ndani yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana udhalimu uliotendwa juu ya Lebanoni utakufunikiza, na kuangamizwa kwao wanyama kutakutia hofu; kwa sababu ya damu ya watu, na kwa sababu ya udhalimu iliotendwa nchi hii, na mji huu, na watu wote wanaokaa ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maovu uliyoitenda Lebanoni yatakuvamia wewe; uliwaua wanyama, wanyama nao watakutisha. Yote hayo yatakupata wewe, kwa mauaji na dhuluma uliyoitendea dunia, naam, uliyoifanyia miji na wakazi wake wote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika, na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha. Kwa sababu umemwaga damu ya mtu, umeharibu nchi na miji na kila mmoja aliyeko ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ukatili ulioifanyia Lebanoni utakufunika, na uharibifu uliowafanyia wanyama utakutisha. Kwa sababu umemwaga damu ya mtu; umeharibu nchi na miji na kila mmoja aliyeko ndani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana udhalimu uliotendwa juu ya Lebanoni utakufunikiza, na kuangamizwa kwao wanyama kutakutia hofu; kwa sababu ya damu ya watu, na kwa sababu ya udhalimu iliotendwa nchi hii, na mji huu, na watu wote wanaokaa ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maovu uliyoitenda Lebanoni yatakuvamia wewe; uliwaua wanyama, wanyama nao watakutisha. Yote hayo yatakupata wewe, kwa mauaji na dhuluma uliyoitendea dunia, naam, uliyoifanyia miji na wakazi wake wote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani makorofi, ambayo uliitendea Libanoni, yatakufunika, nao nyama, uliowaua bure tu, watakutia woga, kwa ajili ya damu za watu, ulizozimwaga kwa kuikorofisha nchi na miji pamoja na wenyeji wao wote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana udhalimu uliotendwa juu ya Lebanoni utakufunikiza, na kuangamizwa kwao wanyama kutakutia hofu; kwa sababu ya damu ya watu, na kwa sababu ya udhalimu iliotendwa nchi hii, na mji huu, na watu wote wanaokaa ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mateso uliyoyatenda kule Lebanoni yatakulemea wewe; uliwaua nyama, nyama nao watakuogopesha. Yote hayo yatakupata wewe, kwa mauaji na mateso uliyoitendea dunia, uliyoifanyia miji na wakaaji wake wote.