Habakkuk 2:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Chafaa nini kinyago alichotengeneza mtu? Sanamu ni madini yaliyoyeyushwa, ni kitu cha kueneza udanganyifu! Mtengeneza sanamu hutumaini alichotengeneza mwenyewe, kinyago ambacho hakiwezi hata kusema!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sanamu ina thamani gani, kwani mwanadamu ndiye alichonga? Ama kinyago kinachofundisha uongo? Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe; hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sanamu ya kuchora yafaa nini, hata yeye aliyeifanya ameichora? Sanamu ya kuyeyuka, nayo ni mwalimu wa uongo, yafaa nini, hata yeye aliyeifanya aiwekee tumaini lake, na kufanya sanamu zisizoweza kusema?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Chafaa nini kinyago alichotengeneza mtu? Sanamu ni madini yaliyoyeyushwa, ni kitu cha kueneza udanganyifu! Mtengeneza sanamu hutumaini alichotengeneza mwenyewe, kinyago ambacho hakiwezi hata kusema!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sanamu ina thamani gani, kwani mwanadamu ndiye aliyechonga? Ama kinyago kinachofundisha uongo? Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe; hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sanamu ina thamani gani, kwani mwanadamu ndiye alichonga? Ama kinyago kinachofundisha uongo? Kwa kuwa yeye aliyekitengeneza hutegemea kazi ya mikono yake mwenyewe; hutengeneza sanamu zisizoweza kuzungumza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sanamu ya kuchonga yafaa nini, baada ya aliyeifanya ameichonga? Sanamu ya kuyeyuka, nayo ni mwalimu wa uongo, yafaa nini, hata yeye aliyeifanya aiwekee tumaini lake, na kufanya sanamu zisizoweza kusema?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Chafaa nini kinyago alichotengeneza mtu? Sanamu ni madini yaliyoyeyushwa, ni kitu cha kueneza udanganyifu! Mtengeneza sanamu hutumaini alichotengeneza mwenyewe, kinyago ambacho hakiwezi hata kusema!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo kinyago kilichochongwa kitafaaje? Maana ni kazi tu ya fundi aliyekichonga. Au kinyago cha vyuma vilivyoyeyushwa kifundishacho uwongo tu kitafaaje? Maana ni egemeo lake fundi aliyekitengeneza, apate miungu isiyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sanamu ya kuchora yafaa nini, hata yeye aliyeifanya ameichora? Sanamu ya kuyeyuka, nayo ni mwalimu wa uongo, yafaa nini, hata yeye aliyeifanya aiwekee tumaini lake, na kufanya sanamu zisizoweza kusema?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sanamu mutu aliyotengeneza inafaa kwa nini? Sanamu ni madini yaliyoyeyushwa, ni kitu cha kueneza udanganyifu! Mutengenezaji wa sanamu anatumainia kile alichotengeneza mwenyewe, sanamu ambayo haiwezi hata kusema!