Habakkuk 3:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bwana, Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu, huiimarisha miguu yangu kama ya paa, huniwezesha kupita juu milimani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bwana Mungu Mwenyezi ni nguvu yangu; huifanya miguu yangu kama miguu ya ayala, huniwezesha kupita juu ya vilima. Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bwana, Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu, huiimarisha miguu yangu kama ya paa, huniwezesha kupita juu milimani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mwenyezi ni nguvu yangu; huifanya miguu yangu kama miguu ya paa, huniwezesha kupita juu ya vilima. (Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenyezi ni nguvu yangu; huifanya miguu yangu kama miguu ya ayala, huniwezesha kupita juu ya vilima. Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
MUNGU, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bwana, Mwenyezi-Mungu ndiye nguvu yangu, huiimarisha miguu yangu kama ya paa, huniwezesha kupita juu milimani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu ndiye aliye nguvu yangu! Anipa miguu ipigayo mbio kama yake kulungu, akiniendesha vema, nifike juu vilimani kwangu. Kwa mwimbishaji, ayaimbie mazeze yangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
YEHOVA, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Bwana, Yawe ndiye nguvu yangu, anaimarisha miguu yangu kama ya paa, ananiwezesha kupita juu katika milima. Kwa mwimbishaji: pamoja na ala za muziki wa nyuzi.