Habakkuk 3:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akisimama dunia hutikisika; akiyatupia jicho mataifa, hayo hutetemeka. Milima ya milele inavunjwavunjwa, vilima vya kudumu vinadidimia; humo zimo njia zake za kale na kale.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alisimama, akaitikisa dunia; alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke. Milima ya zamani iligeuka mavumbi na vilima vilivyozeeka vikaanguka. Njia zake ni za milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akasimama, akaitetemesha dunia; Akatazama, akawasitusha mataifa; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akisimama dunia hutikisika; akiyatupia jicho mataifa, hayo hutetemeka. Milima ya milele inavunjwavunjwa, vilima vya kudumu vinadidimia; humo zimo njia zake za kale na kale.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alisimama, akaitikisa dunia; alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke. Milima ya zamani iligeuka mavumbi na vilima vilivyozeeka vikaanguka. Njia zake ni za milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alisimama, akaitikisa dunia; alitazama, na kuyafanya mataifa yatetemeke. Milima ya zamani iligeuka mavumbi na vilima vilivyozeeka vikaanguka. Njia zake ni za milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akasimama na kuitikisa dunia; Akatazama, mataifa yakatetemeka; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akisimama dunia hutikisika; akiyatupia jicho mataifa, hayo hutetemeka. Milima ya milele inavunjwavunjwa, vilima vya kudumu vinadidimia; humo zimo njia zake za kale na kale.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Anaposimama ndipo, anapoitetemesha nchi; anapochungulia ndipo, anapoyastusha mataifa. Milima iliyoko toka kale huatuka, vilima vilivyoko kale na kale huangukiana chini; ni vilevile, alivyovikanyaga juu tangu kale alipopita.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akasimama, akaitetemesha dunia; Akatazama, akawasitusha mataifa; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akisimama dunia inatikisika; akiyatupia mataifa jicho, hayo yanatetemeka. Milima ya milele inavunjwavunjwa, vilima vya zamani za kale vinaanguka; ni juu yao kulipokuwa njia zake za kale na kale.