Haggai 1:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndipo Zerubabeli mwana wa Shealtieli, na kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na watu wote waliokuwa wamerudi kutoka uhamishoni wakafanya kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wao alivyowaambia na kama walivyoambiwa na nabii Hagai, kama alivyotumwa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Watu wakamcha Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua kuhani mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa na Mwenyezi Mungu, Mungu wao. Watu walimwogopa Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hayo mabaki yote ya watu, wakaitii sauti ya Bwana, Mungu wao, na maneno ya Hagai nabii, kama Bwana, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndipo Zerubabeli mwana wa Shealtieli, na kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na watu wote waliokuwa wamerudi kutoka uhamishoni wakafanya kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wao alivyowaambia na kama walivyoambiwa na nabii Hagai, kama alivyotumwa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Watu wakamcha Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua Kuhani Mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti ya BWANA Mungu wao pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa na BWANA Mungu wao. Watu walimwogopa BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua kuhani mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti ya bwana Mwenyezi Mungu wao pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa na bwana Mwenyezi Mungu wao. Watu walimwogopa bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hao watu wote waliokuwa wamebaki, wakaitii sauti ya BWANA, Mungu wao, na maneno ya nabii Hagai, kama BWANA, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndipo Zerubabeli mwana wa Shealtieli, na kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na watu wote waliokuwa wamerudi kutoka uhamishoni wakafanya kama Mwenyezi-Mungu, Mungu wao alivyowaambia na kama walivyoambiwa na nabii Hagai, kama alivyotumwa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Watu wakamcha Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, Zerubabeli, mwana wa Saltieli, na mtambikaji mkuu Yosua, mwana wa Yosadaki, nayo masao yote ya huo ukoo walipoisikia sauti ya Bwana Mungu wao nayo maneno ya mfumbuaji Hagai, Bwana Mungu aliyemtuma kuwaambia hayo, nao wa ukoo huu wakamwogopa Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hayo mabaki yote ya watu, wakaitii sauti ya BWANA, Mungu wao, na maneno ya Hagai nabii, kama BWANA, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu Zerubabeli mwana wa Saltieli, na Kuhani Mukubwa Yoshua mwana wa Yosadaki, pamoja na watu wote waliokuwa wamerudi kutoka katika uhamisho wakafanya kama vile Yawe, Mungu wao alivyowaambia na kama vile walivyoambiwa na Hagai, yule nabii aliyetumwa na Yawe, Mungu wao. Watu wakamuheshimia Yawe.