Haggai 1:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, Mwenyezi-Mungu akawapa moyo Zerubabeli mkuu wa Yuda, kuhani mkuu Yoshua na watu wote waliokuwa wamerudi kutoka uhamishoni, walishughulikie hekalu. Walianza kazi hiyo ya kulijenga upya hekalu la Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho za mabaki yote ya watu. Walikuja, wakaanza kufanya kazi katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wao,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho zao mabaki ya watu; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya Bwana wa majeshi, Mungu wao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, Mwenyezi-Mungu akawapa moyo Zerubabeli mkuu wa Yuda, kuhani mkuu Yoshua na watu wote waliokuwa wamerudi kutoka uhamishoni, walishughulikie hekalu. Walianza kazi hiyo ya kulijenga upya hekalu la Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo BWANA akachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya Kuhani Mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho ya mabaki yote ya watu. Walikuja wakaanza kufanya kazi katika nyumba ya BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wao,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo bwana akachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho za mabaki yote ya watu. Walikuja wakaanza kufanya kazi katika nyumba ya bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wao,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho za watu waliokuwa wamebaki; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya BWANA wa majeshi, Mungu wao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, Mwenyezi-Mungu akawapa moyo Zerubabeli mkuu wa Yuda, kuhani mkuu Yoshua na watu wote waliokuwa wamerudi kutoka uhamishoni, walishughulikie hekalu. Walianza kazi hiyo ya kulijenga upya hekalu la Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Bwana akaiamsha roho ya mtawala nchi ya Yuda Zerubabeli, mwana wa Saltieli, nayo roho ya mtambikaji mkuu Yosua, mwana wa Yosadaki, nazo roho zao masao yote ya ukoo huu, wakaenda kufanya kazi ya kuijenga Nyumba ya Bwana Mwenye vikosi aliyekuwa Mungu wao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA akaiamsha roho ya Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda, na roho ya Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, na roho zao mabaki ya watu; wakaenda, wakafanya kazi katika nyumba ya BWANA wa majeshi, Mungu wao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, Yawe akamutia moyo mutawala Zerubabeli wa Yuda pamoja na Kuhani Mukubwa Yoshua na watu wote waliokuwa wamerudi kutoka katika uhamisho. Wakaanza kazi hiyo ya kuijenga upya nyumba ya Yawe wa majeshi, Mungu wao,