Haggai 1:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mlitazamia mavuno mengi, lakini mlipata kidogo tu. Na mlipoyaleta nyumbani, niliyapeperusha mbali. Kwa nini? Kwa sababu hekalu langu ni magofu matupu hali kila mmoja wenu anashughulikia nyumba yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mlitarajia mengi, kumbe, yametokea kidogo. Ulichokileta nyumbani nilikipeperusha. Kwa nini?” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Ni kwa sababu ya nyumba yangu, inayobaki katika hali ya magofu, wakati kila mmoja wenu anajishughulisha na nyumba yake mwenyewe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema Bwana wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mlitazamia mavuno mengi, lakini mlipata kidogo tu. Na mlipoyaleta nyumbani, niliyapeperusha mbali. Kwa nini? Kwa sababu hekalu langu ni magofu matupu hali kila mmoja wenu anashughulikia nyumba yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mlitarajia mengi, kumbe, yametokea kidogo. Ulichokileta nyumbani nilikipeperusha. Kwa nini?” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote. “Ni kwa sababu ya nyumba yangu, inayobaki katika hali ya magofu, wakati kila mmoja wenu anajishughulisha na nyumba yake mwenyewe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mlitarajia mengi, kumbe, yametokea kidogo. Ulichokileta nyumbani nilikipeperusha. Kwa nini?” asema bwana Mwenye Nguvu Zote. “Ni kwa sababu ya nyumba yangu, inayobaki katika hali ya magofu, wakati kila mmoja wenu anajishughulisha na nyumba yake mwenyewe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha mbali. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu yumba yangu imebaki kuwa gofu la nyumba, wakati ambapo kila mmoja wenu anakimbilia nyumbani kwake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mlitazamia mavuno mengi, lakini mlipata kidogo tu. Na mlipoyaleta nyumbani, niliyapeperusha mbali. Kwa nini? Kwa sababu hekalu langu ni magofu matupu hali kila mmoja wenu anashughulikia nyumba yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mliwaza kupata mengi, lakini mlipoyatazama, yalikuwa machache, nayo mliyoyapeleka nyumbani, nikayapeperusha; hivyo ni kwa sababu gani? ndivyo, aulizavyo Bwana Mwenye vikosi. Ni kwa ajili ya Nyumba yangu iliyo hame tu, nanyi mnajihimiza kila mtu kuijenga nyumba yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache; tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia kila mtu nyumbani kwake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mulitazamia mavuno mengi, lakini mulipata kidogo tu. Mulipoyaleta kwenye nyumba, niliyapeperusha mbali. Kwa nini? Kwa sababu nyumba yangu ni mabomoko matupu wakati kila mumoja wenu anashugulikia nyumba yake.