Haggai 2:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnamo siku ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, katika mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Mwenyezi-Mungu wa majeshi lilimjia nabii Hagai,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, katika mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Mwenyezi Mungu lilikuja kwa nabii Hagai:
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku ya ishirini na nne, ya mwezi wa kenda, katika mwaka wa pili wa Dario, neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha Hagai nabii, kusema,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnamo siku ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, katika mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Mwenyezi-Mungu wa majeshi lilimjia nabii Hagai,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, katika mwaka wa pili wa utawala Mfalme Dario, neno la BWANA lilikuja kwa nabii Hagai:
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno la bwana lilikuja kwa nabii Hagai:
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku ya ishirini na nne, ya mwezi wa tisa, katika mwaka wa pili wa Dario, neno la BWANA lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnamo siku ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, katika mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Mwenyezi-Mungu wa majeshi lilimjia nabii Hagai,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa katika mwaka wa pili wa Dario neno la Bwana likaja kwa msaada wa mfumbuaji Hagai la kwamba:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku ya ishirini na nne, ya mwezi wa kenda, katika mwaka wa pili wa Dario, neno la BWANA lilikuja kwa kinywa cha Hagai nabii, kusema,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Katika siku ya makumi mbili na ine ya mwezi wa kenda, katika mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Yawe wa majeshi lilimufikia nabii Hagai kusema hivi: