Haggai 2:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Hagai akawaambia, “Mwenyezi-Mungu asema kwamba, hivyo ndivyo ilivyo kwa watu wa taifa hili na kila kitu wanachofanya; kadhalika na kila wanachotoa madhabahuni ni najisi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha Hagai akasema, “ ‘Basi ndivyo walivyo machoni pangu hawa watu na taifa hili,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Lolote wafanyalo na chochote watoacho hapo ni najisi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo Hagai akajibu, akasema, Hivyo ndivyo walivyo watu hawa, na hivyo ndivyo lilivyo taifa hili mbele zangu, asema Bwana; na hivyo ndivyo ilivyo kila kazi ya mikono yao; na kitu hicho wakitoacho sadaka huko ni najisi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Hagai akawaambia, “Mwenyezi-Mungu asema kwamba, hivyo ndivyo ilivyo kwa watu wa taifa hili na kila kitu wanachofanya; kadhalika na kila wanachotoa madhabahuni ni najisi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha Hagai akasema, “ ‘Basi ndivyo walivyo machoni pangu hawa watu na taifa hili,’ asema BWANA. ‘Lo lote wafanyalo na cho chote watoacho hapo ni najisi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha Hagai akasema, “ ‘Basi ndivyo walivyo machoni pangu hawa watu na taifa hili,’ asema bwana. ‘Lolote wafanyalo na chochote watoacho hapo ni najisi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo Hagai akajibu, akasema, Hivyo ndivyo walivyo watu hawa, na hivyo ndivyo lilivyo taifa hili mbele zangu, asema BWANA; na hivyo ndivyo ilivyo kila kazi ya mikono yao; na kitu hicho wakitoacho sadaka huko ni najisi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Hagai akawaambia, “Mwenyezi-Mungu asema kwamba, hivyo ndivyo ilivyo kwa watu wa taifa hili na kila kitu wanachofanya; kadhalika na kila wanachotoa madhabahuni ni najisi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hagai akajibu, akasema: Ndivyo, asemavyo Bwana: Ndivyo walio ukoo huu walivyo, ndivyo hili taifa lilivyo machoni pangu, ndivyo nazo kazi zote za mikono yao zilivyo, ndivyo navyo vipaji vyote wanavyonitolea vilivyo, vyote ni vichafu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo Hagai akajibu, akasema, Hivyo ndivyo walivyo watu hawa, na hivyo ndivyo lilivyo taifa hili mbele zangu, asema BWANA; na hivyo ndivyo ilivyo kila kazi ya mikono yao; na kitu hicho wakitoacho sadaka huko ni najisi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hagai akajibu na kusema hivi: Hivi ndivyo inavyokuwa kwa watu wa taifa hili mbele yangu –ni ujumbe wa Yawe– na kila kitu wanachofanya; hata vitu wanavyotoa kwenye mazabahu ni vichafu.