Haggai 2:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo, nitakuchukua wewe mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli, na kukuteua ili utawale kwa jina langu. Wewe ndiwe niliyekuchagua.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi amesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“ ‘Katika siku ile,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, ‘nitakuchukua wewe, mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Nitakufanya kama pete yangu ya muhuri, kwa kuwa nimekuchagua,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika siku ile, asema Bwana wa majeshi, nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa Shealtieli, asema Bwana, nami nitakufanya kuwa kama pete yenye muhuri; kwa kuwa nimekuchagua, asema Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo, nitakuchukua wewe mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli, na kukuteua ili utawale kwa jina langu. Wewe ndiwe niliyekuchagua.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi amesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“ ‘Katika siku ile,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote, ‘nitakuchukua wewe, mtumishi wangu Zerubabeli, mwana wa Shealtieli,’ asema BWANA. ‘Nitakufanya kama pete yangu ya muhuri, kwa kuwa nimekuchagua,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“ ‘Katika siku ile,’ asema bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nitakuchukua wewe, mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli,’ asema bwana. ‘Nitakufanya kama pete yangu ya muhuri, kwa kuwa nimekuchagua,’ asema bwana Mwenye Nguvu Zote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa Shealtieli, asema BWANA, nami nitakufanya kuwa kama pete yenye mhuri; kwa kuwa nimekuchagua, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo, nitakuchukua wewe mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli, na kukuteua ili utawale kwa jina langu. Wewe ndiwe niliyekuchagua.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi amesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi: Siku hiyo ndipo, nitakapokuchukua wewe Zerubabeli, mwana wa Saltieli, kwa kuwa u mtumishi wangu; ndivyo, asemavyo Bwana. Nitakutunza kama pete yangu yenye muhuri, kwani nimekuchagua; ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, nitakutwaa wewe, Ee Zerubabeli, mtumishi wangu, mwana wa Shealtieli, asema BWANA, nami nitakufanya kuwa kama pete yenye muhuri; kwa kuwa nimekuchagua, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo, nitakutwaa wewe Zerubabeli mwana wa Saltieli, mutumishi wangu. –Ni ujumbe wa Yawe wa majeshi! Nitakusimika utawale kwa jina langu. –Ni ujumbe wa Yawe! Wewe ndiwe niliyekuchagua. –Ni ujumbe wa Yawe wa majeshi!