Haggai 2:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata hivyo, usife moyo, ewe Zerubabeli. Jipe moyo, kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki. Jipeni moyo nanyi watu wote wa nchi hii. Fanyeni kazi, maana mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nipo pamoja nanyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa uwe imara, ee Zerubabeli,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Kuwa imara, ee kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki. Mwe imara, enyi watu wote wa nchi,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘na mfanye kazi. Kwa kuwa mimi nipo pamoja nanyi,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sasa uwe hodari, Ee Zerubabeli, asema Bwana; nawe uwe hodari, Ee Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, nanyi iweni hodari, enyi watu wote wa nchi hii, asema Bwana; mkafanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi, asema Bwana wa majeshi;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata hivyo, usife moyo, ewe Zerubabeli. Jipe moyo, kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki. Jipeni moyo nanyi watu wote wa nchi hii. Fanyeni kazi, maana mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nipo pamoja nanyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa uwe imara, Ee Zerubabeli,’ asema BWANA. ‘Kuwa imara, Ee Kuhani Mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki. Muwe imara, enyi watu wote wa nchi,’ asema BWANA, ‘na mfanye kazi. Kwa kuwa mimi nipo pamoja nanyi,’ asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa uwe imara, ee Zerubabeli,’ asema bwana. ‘Kuwa imara, ee kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki. Mwe imara, enyi watu wote wa nchi,’ asema bwana, ‘na mfanye kazi. Kwa kuwa mimi nipo pamoja nanyi,’ asema bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sasa uwe hodari, Ee Zerubabeli, asema BWANA; nawe uwe jasiri, Ee Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, nanyi iweni jasiri, enyi watu wote wa nchi hii, asema BWANA; mkafanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi, asema BWANA wa majeshi;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata hivyo, usife moyo, ewe Zerubabeli. Jipe moyo, kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki. Jipeni moyo nanyi watu wote wa nchi hii. Fanyeni kazi, maana mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nipo pamoja nanyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana: Sasa Zerubabeli, jipe moyo! Nawe mtambikaji mkuu Yosua, mwana wa Yosadaki, jipe moyo! Nanyi nyote mlio ukoo wa nchi hii, jipeni mioyo! Ndivyo, asemavyo Bwana: Fanyeni kazi, kwani mimi niko pamoja nanyi! ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sasa uwe hodari, Ee Zerubabeli, asema BWANA; nawe uwe hodari, Ee Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, nanyi iweni hodari, enyi watu wote wa nchi hii, asema BWANA; mkafanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi, asema BWANA wa majeshi;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata hivyo, ujipe moyo, ewe Zerubabeli. –Ni ujumbe wa Yawe. Ujipe moyo, Kuhani Mukubwa Yoshua mwana wa Yosadaki. Mujipe moyo nanyi watu wote wa inchi hii. –Ni ujumbe wa Yawe! Mufanye kazi, maana mimi niko pamoja nanyi. –Ni ujumbe wa Yawe wa majeshi!