Hebrews 1:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utazikunjakunja kama joho, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe hubadiliki, nayo miaka yako haikomi kamwe.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Utavikunja hivyo kama koti, navyo vitabadilishwa kama mavazi. Lakini wewe hubadiliki, na uhai wako hautafikia mwisho.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Utazikung'utakung'uta kama joho, kama vazi zitachakaa. Bali wewe hubadiliki, wala miaka yako kamwe haitakoma.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Utazikung’utakung’uta kama joho, nazo zitachakaa kama vazi. Lakini wewe hubadiliki, nayo miaka yako haikomi kamwe.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama mavazi utazikunjakunja, na kama mavazi zitabadilishwa; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nawe utazizinga kama nguo ya kujitandia; zitachujuka kama nguo. Lakini wewe ndiwe yuleyule uliyekuwa, miaka yako haitakoma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; Lakini wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utavikunjakunja kama kanzu, navyo vitabadilishwa kama nguo. Lakini wewe utabaki sawasawa, na maisha yako hayatakuwa na mwisho.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
na kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika; lakini wewe u yeye yule, na miaka yako haitakoma.