Hebrews 1:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yeye ni mngao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwatakasa binadamu dhambi zao, ameketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Baada ya kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Huyo Mwana huuonesha utukufu wa Mungu. Yeye ni nakala halisi ya asili yake Mungu, na huviunganisha vitu vyote pamoja kwa amri yake yenye nguvu. Mwana aliwasafisha watu kutoka katika dhambi zao. Kisha akaketi upande wa kuume wa Mungu, aliye Mkuu huko Mbinguni.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yeye ni mng'ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwapatia binadamu msamaha wa dhambi zao, aliketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yeye ni mng'ao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwatakasa binadamu dhambi zao, ameketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mwana ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko mbinguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mwenyezi Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yeye kwa kuwa ni mng'ao wa utukufu wa Mungu na chapa kamili ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi katika mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yeye ni mngao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwatakasa binadamu dhambi zao, ameketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huyu hutuangazia utukufu wake, kwani kama Mungu alivyo, ndivyo, naye alivyo; tena yeye huvitunza vyote kwa Neno lake lenye nguvu. Alipokwisha kutupatia osho liyaondoalo makosa, akaketi kuumeni kwa mwenye ukuu mbinguni juu,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivichukua vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yeye ni kitambulisho cha mwangaza wa utukufu wa Mungu, kwa maana yeye ni mufano kamili pahali ya Mungu mwenyewe, na kwa uwezo wa neno lake analinda vitu vyote. Naye alipokwisha kuwatakasa watu toka katika zambi zao, aliikaa na mamlaka katika mbingu kwa kuume kwa Mungu Mwenye Uwezo wote.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;