Hebrews 1:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Wewe ni Mwanangu; mimi leo nimekuwa Baba yako.” Wala hakusema juu ya malaika yeyote: “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana ni kwa malaika yupi Mungu aliwahi kusema, “Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuwa Baba yako”? Au tena, “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu”?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu kamwe hajamwambia malaika yeyote maneno haya: “Wewe ni Mwanangu. Mimi leo hii nimekuwa Baba yako.” Mungu pia kamwe hajasema juu ya malaika, “Nitakuwa Baba yake, naye atakuwa mwanangu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Wewe ni Mwanangu; Mimi leo nimekuwa Baba yako.” Wala hakusema juu ya malaika yeyote: “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Wewe ni Mwanangu; mimi leo nimekuwa Baba yako.” Wala hakusema juu ya malaika yeyote: “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana ni malaika yupi ambaye wakati wo wote Mungu alipata kumwambia, “Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuzaa?” Au tena, “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana ni malaika yupi ambaye wakati wowote Mwenyezi Mungu alipata kumwambia, “Wewe ni Mwanangu; leo mimi nimekuzaa”? Au tena, “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu”?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana ni kwa malaika yeyote yupi Mungu alisema, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Wewe ni Mwanangu; mimi leo nimekuwa Baba yako.” Wala hakusema juu ya malaika yeyote: “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani yuko malaika, Mungu aliyemwambia siku iwayo yote: Wewe ndiwe Mwanangu, siku hii ya leo mimi nimekuzaa? Na tena: Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa? Na tena Mimi nitakuwa kwake baba, Na yeye atakuwa kwangu mwana?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Mungu hakumwambia hata mara moja mumoja wa wamalaika wake hivi: “Wewe ni mwana wangu, mimi leo nimekuwa baba yako.” Wala hakusema maneno haya juu ya malaika yeyote: “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwana wangu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana alimwambia malaika yupi wakati wo wote, Mwana wangu ndiwe, mimi leo nimekuzaa? na tena, Mimi nitakuwa kwake baba, na yeye kwangu mwana?