Hebrews 1:7 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kuhusu malaika, alisema: “Amewafanya malaika wake kuwa upepo, na wahudumu wake ndimi za moto.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Anaponena kuhusu malaika, anasema, “Huwafanya malaika wake kuwa pepo, watumishi wake kuwa miali ya moto.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kwa habari za malaika asema,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivi ndivyo Mungu alivyosema kuhusu malaika: “Yeye huwabadilisha malaika zake kuwa upepo na watumishi wake kuwa miali ya moto.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kuhusu malaika, Mungu alisema: “Mungu awafanya malaika wake kuwa pepo, na watumishi wake kuwa ndimi za moto.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kuhusu malaika, alisema: “Amewafanya malaika wake kuwa upepo, na wahudumu wake ndimi za moto.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Anenapo kuhusu malaika husema, “Huwafanya malaika zake kuwa upepo, watumishi wake kuwa miali ya moto.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Anenapo kuhusu malaika asema, “Huwafanya malaika wake kuwa pepo, watumishi wake kuwa miali ya moto.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kuhusu malaika asema, Awafanya malaika wake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kuhusu malaika, alisema: “Amewafanya malaika wake kuwa upepo, na wahudumu wake ndimi za moto.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mambo ya malaika anayasema kwamba: Huwatumia malaika zake kuwa upepo nao watumishi wake kuwa mioto iwakayo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kwa habari za malaika asema, Afanyaye malaika wake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa miali ya moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini juu ya wamalaika, Mungu alisema: “Mungu anawafanya wamalaika wake kuwa kama upepo. Anawafanya hao watumishi wake kuwa kama ndimi za moto.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na katika khabari za malaika anena, Afanyae malaika zake kuwa pepo, na watumislii wake ndimi za moto.