Hebrews 1:8 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini kuhusu Mwana, Mungu alisema: “Kiti chako cha enzi, ee Mungu, chadumu milele na milele! Wewe wawatawala watu wako kwa haki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini kwa habari za Mwana asema, “Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitadumu milele na milele, nayo haki itakuwa fimbo ya utawala ya ufalme wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kwa habari za Mwana asema,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini hivi ndivyo alivyosema kuhusu Mwana wake: “Mungu, ufalme wako utadumu milele na milele. Unatumia mamlaka yako kwa haki.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini kumhusu Mwana, Mungu alisema: “Utawala wako ee Mungu, wadumu milele na milele! Wewe wawatawala watu wako kwa haki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini kuhusu Mwana, Mungu alisema: “Kiti chako cha enzi, ee Mungu, chadumu milele na milele! Wewe wawatawala watu wako kwa haki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kwa habari za Mwana asema, “Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitadumu milele na milele, nayo haki itakuwa fimbo ya utawala ya ufalme wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kwa habari za Mwana asema, “Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitadumu milele na milele, nayo haki itakuwa fimbo ya utawala ya ufalme wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kuhusu Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini kuhusu Mwana, Mungu alisema: “Kiti chako cha enzi, ee Mungu, chadumu milele na milele! Wewe wawatawala watu wako kwa haki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mambo ya mwana anayasema kwamba: Mungu, kiti chako cha kifalme kiko kale na kale pasipo mwisho, nayo fimbo ya ufalme wako ndiyo fimbo inyoshayo mambo ya watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini juu ya Mwana, Mungu alisema: “Kiti chako cha kifalme, Ee Mungu, kitadumu hata milele. Unatawala ufalme wako kwa haki.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini katika khabari ya Mwana anena, Kiti chako, Mungu, ni cha milele; na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya kunyoka.